Swali: Mwanamke ameamka kwa ajili ya kuswali Fajr baada ya kuchomoza kwa jua na akaona kuwa amepata ada yake ya mwezi. Ni kipi kinachomlazimu?Jibu: Ni lazima kwake kulipa swalah ya Fajr iliyompita. Kimsingi ni kwamba damu haikutoka. Mambo yakishakuwa kwamba kimsingi ni kutotoka kwa damu, basi ina maana kwamba alipata hedhi kabla wakati wa swalah kumalizika. Hata hivyo inanisikitikisha kwamba ameamka baada ya kuchomoza kwa jua. Ni wajibu kwa mtu kufanya kila aliwezalo aweze kuamka na kuswali ndani ya wakati.