Swali: Je, inafaa kuwapa swadaqah na zakaah kwa wasiokuwa waislamu?Jibu: Ndio, inafaa kuwapa swadaqah wasiokuwa waislamu kwa ajili ya kuwavuta katika Uislamu ikiwa kuna matarajio ya kusilimu kwao. Ni mamoja pesa hiyo inatokana na zakaah au swadaqah ya kujitolea. Wasiokuwa hao inafaa kuwapa swadaqah ya kujitolea na sio halali kwao zakaah. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu – hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu.”[1]Kuhusu zakaah sio halali kwa kafiri isipokuwa ikiwa ni kwa ajili ya kumlainisha. Amesema (Ta´ala) alipokuwa akibainisha wanaostahiki kupewa zakaah:وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ“… na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa] – ni faradhi itokayo kwa Allaah; na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.”[2][1] 60:8[2] 09:60